Friday, August 13, 2010

ETI WANAWAKE WAREMBO HUUA?

Hivi inawezekana kweli kwa mrembo kama huyu?

Jana tulikuwa na ubishi hapa kazini kwangu. Ubishi wenyewe ulikuwa unahusiana na wanawake warembo. Kuna mwenzetu mmoja amedai kuwa eti hawezi kuoa mwanamke mzuri sana kwa sababu atakufa mapema. Aliendelea kusema kuwa mwanamke mzuri kwa sura na umbo, yaani yule anayekubalika kwa viwango vyote na wanaume kuwa ni mzuri, hafai kuolewa bali ni wa kuchezewa tu na wanaume!

Sababu aliyoitoa ni kwamba eti kuoa mwanamke mzuri sana kwa viwango vyote itamletea presha, kwa sababu atakuwa akitamaniwa na kila mwanaume, na mara nyingi kama mume atakua ni mtu wa kipato kidogo, ni rahisi mkewe huyo kuingia katika vishawisi na kutoka nje ya ndoa kwa sababu atakuwa akiwindwa na wanaume wakware.

Alizidi kubainisha kuwa jambo hilo amelifanyia utafiti na kupata ukweli wa kutosha kuwa wanaume wengi waliooa wanawake wazuri kupindukia aidha walifarki kwa maradhi ya moyo wakiwa bado na umri mdogo au wamepata maradhi ya kudumu kama vile presha na kisukari kutokana na hofu ya kuporwa wake zao hao au hata ukimwi.

Hata wale walioachwa na wake zao baada ya kushawaishiwa na wanaume wenye pesa, wengi waliishia kujinyonga au kujiua kwa kunywa sumu, na wengine waliishia kuwa watumiaji wa aidha madawa ya kulevya au matumizi ya pombe kupindukia.

Ukweli ni kwamba kulizuka ubishi mkubwa pale ofisini kati ya wanawake na wanaume kila upande ukitetea upande wake. Nimeona na mie niilete mada hii hapa kibarazani ili kupata maoni ya wasomaji wa kibaraza hiki.

Je jambo hili lina ukweli wowote?

8 comments:

SIMON KITURURU said...

Kuna wasemao:

``Nionyeshe MWANAMKE MZURI na ntakuonyesha mwanaume aliyemchoka´´

Nakumbuka kipindi fulani wakati maeneo niliyokuwepo hasa kwa WANAUME WEUSI ilikuwa ni kawaida kumsifia actress Halle Berry kuwa ni mzuri sana. Kipindi hicho alikuwa ameolewa na Eric Benet.

Watu walikuwa wanashangaa kwa nini Eric Benet ana malaya wengi nje wakati kaoa mwanamke mzuri hivyo.


Kwa kifupi nachojaribu kusema ni kwamba. Siri ya watu saa nyingine si muonekano. Na mwanamke mzuri ukimjua vizuri unaweza kusahau uzuri wake baada ya kustukia ana jamba tu kama kawaida halafu labda hata staili zake za kukupa utamu ni zilezile hakuna jipya zaidi ya kwamba unapenda chakula kipikwacho na hausigeli kuliko chake.

Halafu kwa bahati mbaya hata wanawake wazuri huzeeka baada ya muda na kama ulichompendea ni uzuri wa ujana wake basi makande huchuja utamu.

Anayepata presha ni yule asiyejiamini na moja ya umuhimu na thamaniya maisha yake kayaoanisha sana na mtu na katika hilo ni huyo kimwana adahaniaye ni mzuri. Na kwa kuwa uzuri u jichoni mwa mtu , afaye kwa presha juu ya mtu wala hahitaji limtu udhanialo ni zuri ili afe kwa presha.:-(


Ni mtazamo tu!

Fadhy Mtanga said...

naomba niongee kitu fulani...mie napenda mwanamke mrembo....kama anaua potelea mbali.....

ila kama asemavyo mtakatifu Simon mwanamke mrembo ni kitu cha kawaida tu ingawa kuna wasemao ubaya wa sura ya mwanamke ndo utamu wake...

ashakum si matusi.

kwa heri.

Yasinta Ngonyani said...

Nimewahi pia kumsikia Dr Remmy Ongala akiimba "mke mzuri ni vizuri aolewe na mume mbaya na mume mbaya aoe mke mzuri kwa sababu wote mkiwa wazuri huyu atasema mimi mzuri na huyu atasema mimi mzuri" MMMhhhh, kaazi kwelikweli kusema kweli siamini kama Mungu aliumba kitu kibaya duniani hapa.

emu-three said...

Hivi inawezekana kweli, mnataka nimuache mke wangu hapana, hiyo sio kweli huo ni uzushi tu...mmmmh,

Koero Mkundi said...

Hiyo mineno huwa inasemwa sana, na wanaume wamekuwa wakidanganyana sana juu ya hilo, na ndo sababu unaweza kusikia wanaume wakisema, "huyu sio wa kuoa bali ni wa kuchezea tu" wakimaanisha kuwa mwanamke mzuri ni wa kuchezea na hafai kuolewa.

Na kutokana na dhana hiyo wanaume wengi kasoro Fadhy Mtanga...LOL wanaogopa san wanawake warembo, na ndio man sishangai haya malumbano yaliyotokea ofisini kwa dada maisara ambapo ameona ni vyema atushirikishe.

Kusema kweli jambo hilo linaukweli ndani yake kwani wanume wengi kutokana na hofu za kuogopa kuporwa wake zao wamejikuta wakijipa jaka moyo kiasi cha klupelekea kupata mashinikizo ya damu na kisukari.

Kwani ni mara ngapi tumeshuhudia ndoa za hao wanaoitwa warembo zikiporomoka na kuvunjika katika hali ya kusikitisha? ni aghalabu san ndoa hizi kudumu na hata kama zikidumu hakika ndani zitakuwa zimeoza kabisa.

Mwakati mwingine kuporomoka kwa ndoa hizi huambatana na maafa.... kama hamuamini hebu anzeni kufanya utafiti japo kidogo......

Mzee wa Changamoto said...

Mambo kadhaa niyaonayo hapa
Kwanza ni kutoka kwenye sentensi ya mwanaume huyo kuwa "yaani yule anayekubalika kwa viwango vyote na wanaume kuwa ni mzuri, hafai kuolewa bali ni wa kuchezewa tu na wanaume!"
Mie hutofautiana na wengi nifanyao kazi nao katika tafsiri ya MWANAMKE MREMBO
Kwa maana hiyo, hakuna mwanamke aliye mrembo kwa vigezo vyote ama hata kwa vigezo vingi vya wengi.
Hapa twapata takwimu kulingana na mazingira tuliyopo.
Lakini kama alivyosema Kaka Kitururu, mwanamke huwa mtamanishi unapoonana naye na mrembo unapoishi naye.
Kwa hiyo tafsiri ya MREMBO ndio inayoleta utata hapa
Kisha tafsiri ya kupenda nayo ni balaa. Yaani ule mstari mwembamba kati ya LOVE, LUST na LIKE unaonekana kufifia (kwa lazima ama hiari) machoni mwa wengi
INASIKITISHA
Huwezi kumpenda usiyemjua na kama unamuona na kumtamani na ukadhani unampenda, basi hapo tatizo si uzuri ama urembo uliouona kwani uliutamani tuuu na hukuupenda
MAPENZI (KWA TAFSIRI HALISI) ni zaidi ya muonekano. Ni MAWAZO, MANENO na MATENDO. Na ukishashikwa katika haya, HUTOTOKA
Kwa hiyo anayetoka, anapungukia mengi ya haya (niseme mawili)ama amekutana na MAIGIZO YAKE NA SI MAISHA YAKE na hapo lazima aache ama aachwe
APENDAYE HAACHI na tafsiri ya mapenzi haiji kabla ya kuwa na uliyenaye.
Wengi huamini kuwa katika penzi baada ya kuishi na mtu kwa muda, kupambana na mambo mbalimbali na kuona fikra pevu za aliye naye
NAMI NI MMOJA WAO
NAWAZA KWA SAUTI TUUU!!!!!!!!!!

Ibrah Rahbi said...

Sio kweli inategemea na akili ya mwanamke husika na mazingira yanachangia! mfano mimi naishi Oman huku wanawake karibu wote ni wazuri tu! mazingira ya nchi sio rahisi kumuona mwanamke wa ki oman anazagaa hovyo bila mpango! mimi siungi mkono hoja hiyo inategemea na akili ya mwanamke husika

Anonymous said...

KIPENDACHO ROHO NIDAWA.