Sunday, August 8, 2010

DALILI ZA WANAWAKE NA WANAUME WANAOSALITI NDOA ZAO HIZI HAPA

Hiki nacho ni kisingizio

Dalili za Mke anayetoka nje ya ndoa:

1) Anatembea na vidonge vya majira kwenye mkoba wake, wakati mume amefanyiwa Vasectomy (Kufunga kizazi kwa mwanaume)
2) Anakuwa na namba ya siri ya simu ambayo mume haijui
3) Anatumia muda mwingi anapokwenda sokoni au kufanya manunuzi ya wiki
4) Anajinunulia nguo za gharama zikiwemo nguo za ndani bila kumshirikisha mume
5) Anakuwa akitegemea zaidi ushauri kutoka nje kwa watu wengine zaidi ya mumewe
6) Anaacha kuvaa pete ya ndoa bila sababu
7) Anapopigiwa simu akiwa karibu na mumewe anaizima au kwenda kupokelea nje
8) Anakuwa hajali tena mambo ya familia na hujiamulia mambo yake mwenyewe
9) Ni rahisi sana kusema ‘nipe talaka yangu’ inapotokea kutofautiana hata kwa jambo dogo.
10) Dharau na kejeli kwa mume hujionyesha waziwazi


Dalili za mume anayetoka nje ya ndoa:

1) Unakuta Condom kwenye mkoba wake au kwenye gari lake wakati umefunga kizazi au unatumia vidonge vya majira.
2) Anapunguza au anaacha kabisa kuwa outing na familia yake
3) Unakuta lipstick kwenye kiti cha gari lake ambayo huifahamu
4) Ghafla anataka mjaribu aina mpya ya kufanya mapenzi
5) Anafanya kazi masaa mengi ya ziada lakini malipo hayaonekani kwenye salary slip
6) Hali au anakula kidogo sana nyumbani kwa kuwa ameshakula kwa nyumba ndogo
7) Nguo zake zinanukia manukato (Perfume)ambayo hata huyafahamu
8) Unakuta alama ya lipstick kwenye shati lake
9) Anakuwa na namba ya siri ya simu na wakati mwingine zaidi ya tatu ambazo mke hazijui
10) Anapopigiwa simu akiwa karibu na mkewe anaizima au kwenda kupokelea nje

4 comments:

emu-three said...

Hizi umezigunduaje, au umezitest namna gani, inawezekana kwa kweli, lakini kama una mkeo kwanini utembee na zana, mmmh, unatoa nauli ya daladala inatoka zana...

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Safi sana. Nilisoma kwenye gazeti la udaku juu ya mwanaume aliyedakwa na mkewe akiwa na boksi zima la kondomu garini mwake. Mke alimpongeza mumewe kwa kujijali na kuyajali maisha yao wote.

Japo inawezekana kuwa na mwenzi mmoja tu maishani; soma hapa uone wanasayansi wanasema nini kuhusu uwezekano wa wanaume kutanga nje ya ndoa...http://matondo.blogspot.com/2009/06/are-men-wired-to-cheat.html

Mzee wa Changamoto said...

Umewapa hizi, sasa wata-update waendane na "wakati"

Msema kweli said...

Mimi sikubaliani na hizo dalili za mwanaume! mimi niliwahi kuoa na nilikuwa na mwanamke nje lakini nikifika nyumbani hakuna kinachobadilika hata simu yangu naiacha siting room tena mke wangu ndio anapokea simu zangu,maana yake nilikuwa siwapi namba yangu nayotumia na family wanawake wa nje na nilikuwa natumia line nyingi sio rahisi! na mambo mengi nilikuwa care cha ajabu mimi ndio nilikuja kugundua mke wangu anatoka nje na tukaachana!! my email ibrah4real@gmail.com