Sunday, August 1, 2010

LIKIZO YANGU MIKOA YA KUSINI NA UTAFITI WANGU UCHWARA!

Daraja la Mkapa


Barabara ilikuwa haipitiki

Viunga vya Mtwara

Kimya changu nilikuwa likizo huko mikoa ya kusini. Ilikuwa ni likizo ndefu kidogo ambapo nilipata fursa ya kuwatembelea wakwe zangu niliopoteana nao kwa miaka kadhaa iliyopita.

Pamoja na likizo lakini nilitumia muda wangu kujifunza mambo mengi ambayo kama nitapata fursa, basi nitawashirikisha ili tujadili kwa pamoja.

Hali ya barabara si ya kuridhisha ingawa wenyeji waliniambia kuwa hali kwa sasa ni ya afadhali ukilinganisha na kipindi cha nyuma. Kwa mfano kutoka Ikwiriri lilipo daraja la Mkapa mpaka Somanga ni kama Kilomita 60, na kipande hicho hakina lami, wakati tunakwenda huko kulikua na hali ya mvua hivyo barabara ilikuwa inateleza sana.

Hata hivyo nilivutiwa sana na Daraja la Mkapa ambalo kwa kweli ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuliona tangu lilipojengwa. Kutokana na kuliona daraja hilo, nikajikuta nikihesabu idadi ya madaraja nikianzia Mtwara.

Inawezekana nisiwe sahihi sana lakini kulingana na hesabu zangu nimepata idadi ya madaraja ifuatayo:

Kutoka Mtwara hadi Mnazi Mmoja nilipata idadi ya madaraja 5
Kutoka Mnazi Mmoja hadi Lindi nilipata idadi ya madaraja 6
Kutoka Lindi hadi Kibiti nilipata idadi ya madaraja 79

Pamoja na idadi hiyo ya madaraja, pia yapo yanayojengwa, ambayo ni yale ya kutoka Somanga hadi Daraja la mkapa nilipata idadi ya madaraja 45.
Kutoka Daraja la Mkapa hadi Dar nilipata idadi ya madaraja 17

Ukijumlisha hiyo idadi ya madaraja unapata jumla ya madaraja 152. kwa umbali wa kilomita 554, yaani kutoka Dar hadi Mtwara!

Naambiwa kuwa gharama za ujenzi wa barabara huwa zinakuwa kubwa kulingana na idadi ya madaraja yatakayojengwa. Hapo ndipo nilipowaza kuwa isije kuwa kuchelewa kujengwa kwa barabara za mikoa ya kusini kulichangiwa zaidi na idadi ya madaraja kuwa mengi, ukilinganisha na mikoa mingine hususan ya kaskazini.

Kwa mujibu mdogo wangu Koero ameniambia kuwa kutoka Dar hadi Arusha ni kilomita 659, alinifafanulia kuwa kutoka Dar hadi Moshi ni kilomita 570, na kutoka Moshi hadi Arusha ni kilomita 89, ukijumlisha unapata hizo kilomita 659, ambapo alikanusha pia kuwa hakuna idadi nyingi ya madaraja ukilinganisha na huko mikoa ya kusini.

Ni kautafiti kadogo ambako nimekafanya wakati wa likizo yangu na ndio sababu ya kuweka hapa kibarazani ili mwenye kufahamu zaidi aweke changamoto yake hapa.

Nikipata muda nitawasimulia vijimambo nilivyokutana navyo huko ukweni, si mnanijua siishi visa!

7 comments:

Koero Mkundi said...

Pole na safari bi dada, huu sio utafiti uchwara, bali ni utafiti jaididi.

Nakushauri uwe mkandarasi maana hizo data utadhani ni Mheshimiwa Magufuli anayejua hata idadi ya Sangara katika ziwa Victoria.

nakupongeza sana kwa hilo........

Yasinta Ngonyani said...

Kwanza kabisa napenda kusema karibu tena kwenye ulimwengu huu. Pili nakupa pole kwa safari, ni kweli ulikuwa na kazi ya kuhusabu haya madaraja.....Hongera sana na nasubiri kwa hamu simulizi kutoka kwa wakwe...lol

emu-three said...

Huo ndio utafiti yakinifu, manake unatafiti kivitendo, sio utafiti wa makaratasi, hivi wewe hujajaza karatasi ya kuomba Ubunge, unafaa sana, tunataka wabunge wafuatiliaji sio wafuatiliwao

Markus Mpangala said...

Duh natamani kama ungeendelea kuandika utafiti huu ni bonge la uthibitisho wa hali hiyo. halafu natamani ungesafiri kwenda tunduru halafu kutoka tunduru hadi songea kuanzia mtwara, ni aibu jamani heeeee

chib said...

Barabara nyingine huko ni hatari. Mie ukiniambia kuhesabu sijui nini barabarani, yaani andika zero.

Stephan said...

cool

Dlomen said...

http://lnfaw.blogspot.com/