Sunday, May 23, 2010

NI UREMBO AU?

Ni urembo au?

Linapokuja swala la utamaduni, hasa kwa kuangalia mila zetu sisi Waafrika utakutana na tamaduni nyingi sana zenye kusisimua. Kwa mfano ni kawaida kumkuta Mwanamke wa Kizulu kutoka kule Afrika ya Kusini akiwa amevaa shanga maarufu kama chachandu nje nje na wenyewe wanaliona jambo hili kama kitu cha kawaida. Lakini hebu fikiria hapa Bongo I mean Tanzania mwanamke akiamua kuvaa shanga zake nje nje na kukatiza mitaa……mama weee si mayowe na miluzi hiyo kutoka kwa wanaume utadhani wameona kitu gani sijui..!!

Lakini la kustaajabisha zaidi ni pale baadhi ya wanaume wanapopotosha na kudai kuwa mwanamke kuvaa shanga ni umalaya…..Hapa kunahitajika mjadala mzito ili tuwekane sawa maana kuna baadhi ya mashoga zangu wanaogopa kuvaa kwa kudai kuwa wataonekana ni malaya ilhali ni utamaduni na pia ni kama nakshi au urembo kwa mwanamke.

Je hili nalo mnalionaje………