Saturday, July 10, 2010

UKIMYA WANGU!

Kimya changu, hakika kinamshindo,
Msijedhani nikimya, milele hata dahali,
Kuwa kwangu kimya, ni sawa na ada ya mja,
Ukimya wangu

Ada ya mja hunena, walisema wahenga,
Kwa muungwan ni vitendo, walimalizia malenga,
Kukaa kwangu kimya, hakika ni uungwana,
Ukimya wangu